February 20, 2020


HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa wachezaji wake wanacheza kwa kasi kipindi cha kwanza na kushindwa kumudu kipindi cha pili kutokana na uchovu.

Namungo ilishinda mabao 2-1 mbele ya KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Majaliwa inajiandaa kumenyana na Azam FC iliyotoka kulazimisha sare na Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa wachezaji wake ujanja wao umekuwa ni kipindi cha kwanza kucheza kwa kasi kubwa ila kipindi cha pili mambo huwa tofauti kutokana na uchovu.

"Wamekuwa wakicheza na kusafiri kwa wakati mfupi, hilo limenifanya nije na mbinu mpya kufanya maboresho kwenye kikosi changu, kwa sasa tunajiaandaa na mchezo wetu dhidi ya Azam FC" amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic