February 20, 2020


JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa kichapo cha mabao 2-1 mbele ya Ruvu Shooting kinamhusu yeye kwa kuwa ni kiongozi kwenye benchi la ufundi atapambana kufuta makosa yake kwenye mechi zake zinazofuata.

Mgunda amesema kuwa wamefungwa na wapinzani wao kwa makosa ya uzembe wao wenyewe hivyo hakuna mwingine anayepaswa kulaumiwa zaidi yake na kazi yake itakuwa ni kutafuta majibu ya makosa yao.

"Tumefungwa hilo lipo wazi makosa ni yetu tunachotakiwa kwa sasa ni kusahau yaliyopita na kutafuta majibu ya makosa ambayo tumeyafanya.

"Ushindani ni mkubwa na kila mmoja anapambana kupata matokeo mazuri,mchezo wetu unaofuata tutapambana kupata matokeo mazuri," amesema.

Coastal Union itamenyana na Yanga iliyo chini ya Luc Eymael, Februari 23 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic