February 21, 2020


MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa watawafudisha soka wapinzani wao Polisi Tanzania kwenye mchezo wao wa Lgi Kuu Bara utakaochezwa kesho Uwanja wa Ushirika Moshi.

Bwire amesema kuwa ushindi wa kibabe mbele ya Coastal Union wa mabao 2-1 ni salamu tosha kwa wapinzani wao Polisi Tanzania.

"Tupo Bongo ila tunapiga mpira kama Barcelona sasa unadhani tukikuana na Polisi Tanzania nini kitatokea? Tutawapigia mpira mwingi mpaka watasahau shida zao na kuanza kutushangilia sisi.

"Tunahitaji pointi tatu huu ndio mpango wetu mkubwa mengine yatatokea ndani ya uwanja, mashabiki wajitokeze kwa wingi," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic