February 21, 2020


UONGOZI wa Simba umesema kuwa maadalizi yao ya mchezo wa kesho dhidi ya Biashara United yapo sawa ni suala la wakati tu kutimiza malengo waliyojiwekea.

Simba itaikaribisha Biashara United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Francis Baraza kwenye mchezo wa Ligi Kuu utakaochezwa Uwanja wa Taifa majira ya saa 1:00 usiku.

Akizugumza na Saleh Jembe, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa hali za wachezaji zipo sawa wana imani watafanya vizuri mbele ya Biashara United.

"Wachezaji wanatambua wajibu wao hivyo suala la morali ni kazi yao kutimiza majukumu ndani ya Uwanja, mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu yao," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic