November 30, 2020

 


EDINSON Cavan nyota wa Manchester United anakabiliwa na rungu kutoka Shirikisho la Soka nchini Uingereza (FA) baada ya kuhusishwa na suala la ubaguzi wa rangi kupitia ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa kijamii muda mfupi baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Southampton. 


Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa St Mary's,  Cavan alifunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao baada ya kuingia kipindi cha pili timu yake ilipokuwa nyuma kwa kufungwa mabao 2-0.


Baada ya kutimiza majukumu yake na kuifanya timu yake kushinda mchezo huo aliandika ujumbe uliosomeka 'Gracias negrito' ikiwa inahusiana na ubaguzi ambapo tafsri yake ni 'ninawashukuru weusi'.


Ujumbe huo ambao aliutuma kupitia mtandao wa twita ulikaa muda wa masaa matatu kisha akaufuta huku akisistiza kuwa neno hilo aliliskia likitumika na watu wa Amerika ya Kusini hivyo hana tatizo ikiwa ataadhibiwa.


FA wanafuatilia juu ya ujumbe huo na anaweza kuchukuliwa hatua ya kufungiwa kucheza mechi pamoja na faini ya fedha.

3 COMMENTS:

  1. Huyu nae kumbe boya tuu, inakuwaje uposti neno bila kujua maana yake? Jitu zima kumbe ovyo tuu. Wachezaji wanapiga magoti kila siku wakati wa kuanza michezo ya ligi ya EPL lenyewe linakuwaga wapi lisijue kinachoendelea? Afungiwe tuu hata mechi 8 itapendeza.

    ReplyDelete
  2. Edison Cavan goal gater fitna tu za waingereza wasenge hao wameona spidi yake kali

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic