November 30, 2020


 SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa licha ya kushinda mchezo wa kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa hatua ya awali bado kazi haijaisha lazima wajiweke sawa kwa ajili ya mchezo wa marudio.


Jana, Novemba 29, Simba ilishinda bao 1-0 dhidi ya Plateau United kwenye mchezo wa awali ya Ligi ya Mabingwa nchini Nigeria uliochezwa Uwanja wa New Jos.


Bao la ushindi lilifungwa na nyota Clatous Chama dakika ya 53 kwa pasi ya kiungo mwenzake Luis Miquissone.


Sven amesema:"Wapinzani wetu wana nguvu na walijaribu kiufundi kutafuta goli lakini walishindwa kutokana na uimara wa wachezaji wangu katika hilo ninawapongeza.


 "Matokeo tuliyopta ni mazuri lakini bado hatujamaliza kazi kwa sababu wiki ijayo tuna dakika 90 zingine." amesema.

Mchezo wa marudio kwa timu hizi unatarajiwa kuchezwa Desemba 5, Uwanja wa Mkapa na Simba inahitaji ushindi ama sare ya aina yoyote ili isonge mbele hatua ya mtoano.


3 COMMENTS:

  1. ACHA KUWAZUGA MASHABIKI UNA KAZI NGUMU GANI WAKATI MMEPANGIWA TIMU NYEPESI ROJOROJO ILIYO CHUKUA UBINGWA SABABU YA CORONA, HIYO NI SAWA NA MBAO FC YA TANZANIA ICHUKUE UBINGWA KISA INAONGOZA LIGI MWANZONI NA BAHATI LIGI ISIMAMISHWE GHAFLA NA MBAO WAWE MABINGWA, HAO PLATEAU NI LEVO YA MBAO, JKT TZ MTIBWA NK MSIJIDANGANYE KUNYWENI MTORI NYAMA MTAZIKUTA CHINI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu nyani naye kakurupukia wapi kwani msimu wa mahindi tayari?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic