May 4, 2021


NYOTA wa Simba wameweka wazi kwamba watapambana kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Mei 8, Uwanja wa Mkapa.

Nyota hao ni pamoja na Clatous Chama ambaye ni kinara wa pasi za mwisho akiwa nazo 13 na ametupia mabao 7 pamoja na Luis Miquissone ambaye ametupia mabao 7 na pasi 9 za mabao.

Pia beki wa kati Joash Onyango amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Chama amesema:"Kwetu sisi kila mchezo ni muhimu na kikubwa ni kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu,".

Luis amesema kuwa:"Tunahitaji kufanya vizuri katika mechi zetu zote hivyo hakuna namna tupo tayari kwa ajili ya ushindani,".

Onyango beki kisiki amesema:"Tunaangalia mechi zetu zijazo ambazo ni za karibu hapo tutaanzia kufanya vizuri, kikubwa ni kuona kwamba tunapata pointi tatu," .

Mchezo wao wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 1-1 Simba hivyo Mei 8 utakuwa ni mchezo wa kusaka ushindi ili kujenga ufalme katika kusaka ubingwa wa ligi.

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 61 baada ya kucheza mechi 25, Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 27 hivyo mshindi wa mchezo huo atakuwa anajenga mazingira ya kuelekea ubingwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic