KUELEKEA msimu mpya wa 2021/22 ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara ,(TPLB) imepanga kumaliza zoezi la kukagua viwanja vitakavyotumika ifikapo Agosti 31.
Mtendaji Mkuu wa TPLB, Almas Kasongo amesema kuwa ni lazima timu ziweze kufanya maboresho ya viwanja vyao mapema kabla ya kukaguliwa kwa ajili ya matumizi kwenye mechi zao.
"Timu zote ni lazima zizingatie huo utaratibu wa kufanya marekebisho na kuboresha viwanja vyao mapema kwa ajili ya matumizi.
"Tunatarajia kufikia Agosti 31 timu zote ziwe zimekamilisha zoezi hilo na kwa timu ambazo hazitafuata maelekezo basi zitachukuliwa hatua.
"Mara baada ya ligi kuanza tunataka mazingira yawe sawa ili timu zitakapocheza zicheze katika ubora nyumbani na ugenini," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment