tag:blogger.com,1999:blog-5720843249720986699.post1533410784912172824..comments2023-12-31T11:28:41.093+03:00Comments on SALEH JEMBE: WANACHOFANYA YANGA NA SIMBA KWA KESSY NI USHINDANI WA WATOTO KABISASalehjembehttp://www.blogger.com/profile/05471687508055401147noreply@blogger.comBlogger1125tag:blogger.com,1999:blog-5720843249720986699.post-88028702057027669762016-07-01T13:55:15.983+03:002016-07-01T13:55:15.983+03:00Simba na Yanga zinaweza zisiwe na Tatizo kubwa kwe...Simba na Yanga zinaweza zisiwe na Tatizo kubwa kwenye hili,mwenye tatizo kubwa ni mchezaji mwenyewe.Badala ya kuugeuza mpira kuwa ajira yake,alionyesha mapenzi ya dhahiri kwa Yanga kwa kufanya makosa ya makusudi kwa mwajili wake(Simba) ili kumhujumu na kuisaidia Yanga.Nani amesahau kadi za makusudi kabisa alizokuwa anazitafuta Kessy kwa lazima ili kuisababishia Simba pengo uwanjani?Ilifika hatua hadi timu nzima ya Simba wakiongozwa na golikipa Vincent waliugundua usaliti wake na akapokea mkong'oto toka kwa Vincent.Mchezaji wa aina hiyo aliyeihujumu Timu una haja gani ya kupoteza fedha na kununua kalamu na karatasi kumuandikia barua ya kumruhusu ahame?Asubiri muda wa pingamizi ukifika ataidhinishwa na TFF kwenda Yanga ambako alikuwa anakutumikia huku akiwa bado yupo Simba.<br /><br />Wachezaji limbukeni na washamba aina ya Kessy wapo wengi hapa nchini,ukiangalia hata mikao,picha na mambo mengine aliyokuwa anayafanya akiwa Kambini Uturuki na Yanga,yanamuonesha kuwa ni kijana wa aina gani,pamoja na kipaji alichonacho,amejawa na ushamba uliopitiliza na hajitambui.Hajuwi kuwa mapenzi yake yanaweza kuangamiza kipaji chake kizuri.Badala ya kuzilaumu Simba na Yanga,ni bora mwandishi ukachukua fursa ya kumuambia ukweli mchezaji ili ajitambue,vinginevyo atapotea mapema sana pamoja na kipaji kizuri alichonacho.Anonymousnoreply@blogger.com