Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) linatoa shukrani kwa kampuni ya Coca Cola kwa kukabidhi fulana
800 na mipira 100 kwa ajili ya ngazi ya mashindano ya vijana wenye umri chini
ya miaka 15 ngazi ya mikoa yanayoanza Septemba Mosi mwaka huu.
Coca Cola ndiyo inayodhamini
mashindano hayo yaliyoanzia ngazi ya wilaya ambapo mwaka huu yatachezwa kwa
kanda na baadaye fainali itakayochezwa kuanzia Septemba 7-14 mwaka huu jijini
Dar es Salaam ikishirikisha mikoa 16 itakayokuwa imefanya vizuri katika ngazi
ya kanda.
Kila mkoa utapata fulana 25 na
mipira mitatu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya timu zao kwa ajili ya michuano
hiyo ngazi ya kanda itakayomazika Septemba 6 mwaka huu.
Kanda hizo ni Mwanza itakayokuwa na
timu za mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na
Tabora. Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Singida inaunda Kanda ya
Arusha.
Zanzibar itakuwa na Kaskazini Pemba,
Kusini Pemba na mikoa miwili ya Unguja wakati Kanda ya Dar es Salaam ina Ilala,
Kinondoni, Lindi, Mtwara, Temeke na mkoa mmoja wa Unguja.
Kanda ya Mbeya inaundwa na Iringa,
Katavi, Mbeya, Njombe, Rukwa na Ruvuma wakati Dodoma, Morogoro, Pwani na Tanga
zinaunda Kanda ya Morogoro.
Mwanza itatoa timu nne kucheza hatua
ya fainali wakati kanda nyingine za Arusha timu mbili, Zanzibar (2), Mbeya (3)
na Kanda ya Morogoro itaingiza timu mbili.
Wakati
huo huo, semina ya makocha 32 wa timu za
mikoa zitakazoshiriki michuano ya U15 FIFA Copa Coca-Cola iliyokuwa ikiendeshwa
na mkufunzi Govinder Thondoo kutoka Mauritius inafungwa leo (Agosti 16 mwaka
huu) saa 9 alasiri kwenye ukumbi wa Msimbazi Center, Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment