Kocha Franciscus
‘Hans’ van der Pluijm ametua jijini Dar es Salaam na kukubaliana na Yanga
kuingia mkataba wa miaka miwili.
Mkataba
huo utasainiwa kesho asubuhi na baada ya hapo, Mholanzi huyo anatarajia kufunga
safari kwenda Zanzibar kuiangalia Simba ya Zdravko Logarusic ikicheza fainali
ya Kombe la Mapinduzi.
Halafu
Jumanne, ataingia kwenye pipa kwenda Uturuki kuungana na kikosi cha Yanga
kilicho kambini mjini Antalya.
Kocha
huyo alitua nchini leo saa tatu asubuhi na moja kwa moja akapelekwa hotelini.
Baada ya
hapo, mazungumzo yalifanyika katika hoteli moja saa 5 asubuhi akiwa na watu wa
kamati inayohusiana na masuala ya usajili.
Mazungumzo
kati ya van der Pluijm na viongozi hao wa Yanga yalikatishwa ili kumpa nafasi
ya kupumzika na baadaye saa 10 jioni wakakutana tena.
Ijumaa
iliyopita, Championi kilikuwa chombo cha habari cha kwanza kuandika kuhusu
kocha huyo aliyetengeneza jina nchini Ghana kuanza mazungumzo na Yanga.
Kama Yanga isingemsajili, chaguo la pili alikuwa ni
Lars Olof Mattsson, raia wa Sweden.
Van der
Pluijm alipata mafanikio makubwa akiwa na Berekum Chelsea ya Ghana katika msimu
wa 2012-13 katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kocha huyo Mholanzi amewahi kuvaana na kikosi cha Logarusic wakati wote wakiwa nchini Ghana wakipiga kazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment