July 1, 2014


Kipa Juma Kaseja na Kocha Marcio Maxim oleo wamekutana live na kuanza kufanya kazi pamoja tokea walipoachana mara ya mwisho 2008.

Kaseja alikuwa benchi wakati Stars inafungwa mabao 4-0 dhidi ya Senegal mjini Dakar, baada ya hapo Maximo hakumuita tena licha ya kuwa na kiwango cha juu.
Baada ya hapo, likawa bifu lakini Maximo alipotua nchini kuinoa Yanga alisema bifu limeisha.
Kweli Kaseja naye akaonyesha nidhamu ya juu leo, baada ya waandishi kumbana kuwa azungumze, naye akaondoka na kumfuata Maximo.
Akauliza kama ni sahihi kufanya hivyo, kocha huyo akampa ruhusa, Kaseja akazungumza na baada ya hapo naye akazungumza.
Pia wakati mazoezi yanaendelea, Maximo mara kadhaa alimuita Kaseja na kumuelekeza halikadhalika mazoezi yalipoisha alifanya hivyo.
Inaonyesha kweli no bifu na sasa wanafanya kazi kwa ajili ya mafanikio.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic