Kiungo mwenye kasi wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi
huenda asiivae leo Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu utakaopigwa Uwanja wa
Taifa kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti aliyoyapata juzi Alhamisi
akiwa mazoezini kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Simba ambayo ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo, inakutana
na Mtibwa inayoshikilia nafasi ya tano huku timu hizo zikiwa na kumbukumbu ya
kutoka sare katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Jamhuri, Morogoro.
Okwi alikiri kuwa afya yake siyo nzuri kutokana na
maumivu ya goti aliyopata mazoezini, ambapo bado hajajua kama atacheza dhidi ya
Mtibwa Sugar au la. Hata hivyo imeelezwa atajisikilizia leo kuwa hali yake ikoje.
“Hali yangu siyo nzuri, lakini siwezi kusema moja kwa
moja kama mchezo wa kesho (leo) dhidi ya Mtibwa kwamba sitacheza kwa sababu leo
(jana) nitaenda mazoezini nitamsikiliza mwalimu kwanza nione atanipangia
programu gani.”
Alipoulizwa Dakatari wa Simba, Yassin Gembe kuhusiana na
maendeleo ya nyota huyo aligoma kuzungumza kwa madai ya kufuata taratibu za
klabu na kumtaka mwandishi amtafute Ofisa Habari, Humphrey Nyansio ambaye
hakupatikana.







0 COMMENTS:
Post a Comment