MAREHEMU CHIWANGO (MWENYE SHATI NYEUPE) AKIPOKEA TUZO YA MWANDISHI ALIYETOA MCHANGO MKUBWA KUTOKA KWA KATIBU MKUU WA TFF, MWESIGWA SELESTINE. KULIA NI RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI |
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetuma salamu za
rambirambi kwa familia ya marehem Willie Chiwango aliyefariki dunia mwishoni
mwa wiki na mazishi kufanyika eneo la Buguruni jijini Dar e Salaam.
Katika salam zake, TFF inawapa pole familia ya marehemu, ndugu,
jamaa, marafiki na kusema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini, wako
pamoja katika kipindi hiki cha maombolezo.
Marehemu
Willie Chiwango ni miongoni mwa waandishi wa habari wa michezo wakongwe kabisa,
aliambatana na timu ya taifa ‘Taifa Stars’ iliyoshiriki michuano ya Mataifa
Afrika mwaka 1980 nchini Nigeria.
TFF
ilimpa cheti cha heshima marehemu Chiwango katika zoezi la kuwakumbuka na
kutambua mchango wa viongozi, wachezaji, waandishi wa habari za michezo
waliojitoa katika sekta ya mpira wa miguu nchini.
0 COMMENTS:
Post a Comment