February 11, 2016


Yanga inaondoka kesho saa 11 Alfajiri kwenda Mauritius katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Cercle de Joachim SC.

Kikosi cha Yanga kinaondoka na ndege ya kukodi ya kampuni ya Air Tanzania na itatumia saa nne na ushee angani ikiwa njiani kwenda nchini humo.


Ikiwa nchini humo, ndege hiyo itakuwa imepaki pembeni ikiisubiri Yanga ikiwa mazoezini, ikiwa hotelini hadi siku ya mechi.

Yanga inatarajia kushuka dimbani ikiwa ugenini na itatakiwa kushinda au kufanya vizuri kabla ya mechi ya marudiano jijini Dar es Salaam.


Baada ya mechi hiyo, ndege hiyo itaruka hadi Pemba moja kwa moja kuepuka kupitia jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kambi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic