September 12, 2017


Siku chache baada ya kudaiwa kuwa Kocha wa Mbeya City, Kinah Phiri hayupo klabuni hapo kutokana na sababu ambazo hazijawekwa wazi, sasa jibu limepatikana.

Habari ni kuwa kocha huyo kumbe aliamua kususa kutokana na kudai mishahara yake ya miezi mitano pamoja na fedha nyingine ya malazi ambayo jumla yake ni shilingi milioni 20.

Kutokana na sakata hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala ameamua kuingilia suala hilo kwa kumuita ofisini kwake kocha huyo kisha kuzungumza naye na ndipo Phiri alipoamua kutoa ya moyoni kwa kueleza ukweli wa sakata hilo.

Akizungumza ukweli wa sakata hilo, Makala alisema ni kweli alimuita ofisini kocha huyo na ameshazungumza naye ambapo ameagiza uongozi wa Mbeya City ushughulikie malipo yake hayo na kuwaeleza kuwa hadi kufikia kesho Jumatano saa nne asubuhi, anataka suala hilo liwe limepata muafaka.

Upande wa Phiri amekiri kweli hajalipwa mshahara wake wa miezi mitano lakini mkuu wa mkoa amemuahidi kulifanyia kazi.

Amesisitiza kuwa baada ya kufikia muafaka wa suala hilo, ataomba wajadiliane juu ya mkataba mpya wa yeye kuendelea kuwa kikosini hapo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic