December 12, 2017


Kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi ameshindwa kufanya mazoezi baada ya gari lake "kumzingua".

Gari lake analotumia lilionekana lina hitilafu wakati anajiandaa kuondoka nyumbani kwake.

Baada ya Tshishimbi kuona asingeweza kulitumia gari lake alianza kufanya juhudi kuliwahi basi la klabu, lakini ikashindikana.

"Baadaye alipewa ruhusa kwamba anaweza kupumzika tu kwa leo na kesho ataendelea na mazoezi maana haikuwa na namna," kilieleza chanzo.

Tshishimbi raia wa DR Congo amerejea mazoezini rasmi wiki hii, kabla alikuwa nje kwa zaidi ya wiki mbili akiwa majeruhi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic