March 17, 2018



Baada ya kikosi cha Simba kinachoivaa Al Masry katika mechi ya Kombe la Shirikisho kuonekana kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusiana na kuanzia benchi kwa kiungo Shiza Kichuya.

Simba inaivaa Al Masry hapa POrt Said katika mechi ya Kombe la Shirikisho. Mechi ya kwanza imeisha kwa sare ya 2-2.

Kocha Pierre Lechantre ameonekana kuelewa vizuri kwa nini ameamua Kichuya aanzie nje.

Lechantre amesema Kichuya ana nafasi ya kuingia baadaye kwa kuwa mfumo atakaoanza nao si ule unamruhusu Kichuya kuanza.

“Al Masry ina wachezaji wengi wenye ubora, nimeangalia mechi zao nyingi sana. Najua wanacheza vipi.

“Kipindi cha kwanza lazima tukabe sana na kuhakikisha tunaziba njia zote. Kichuya ni mzuri mnapokuwa mnashambulia, mkiwa na mpira.

“Mnapopoteza mpira, anakuwa chini sana. Sasa mwanzo tunahitaji mtu mzuri hata mnapokuwa hamna mpira na Kotei anaweza kukaba.

“Kichua ana nafasi ya kuingia na hasa dakika thelathini za mwisho ambazo tutahitaji kushambulia zaidi,” alisema.

Awali ilionekana kuwa na maswali mengi kuhusiana na Kichuya kuanzia katika benchi katika ngumu dhidi ya Al Masry. Baada ya dakika kumi kutoka sasa, Simba wataanza safari kutoka hotelini kwenda uwanjani. 



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic