Yanga ilitangaza juzi kuwa itaitisha mkutano na wanahabari jana majira ya saa saba mchana lakini ulishindwa kufanyika kutokana na sababu zisizozuilika.
Kwa taarifa za chini ya kapeti zinaelezwa Mkwasa alipanga kuachia ngazi lakini Yanga wamekanusha taarifa hizo kwa kushindwa kutoa jibu rasmi kuhusiana na sual hilo.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa klabu, Dismas Ten, alisema kuwa hawezi kuzungumzia suala hilo hivi sasa kutokana na kubanwa na maandalizi ya safari kuelekea Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Wolaitta Dicha FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho.
Kupitia Radio One, Ten alisema kuwa si muda mwafaka kuongelea jambo hilo kama litakuwepo litaelezwa rasmi lakini kwa sasa fikra zote zinahamishiwa kwenye mchezo wa kimataifa.
Yanga inatarajia kuondoka muda wowote kuelekea Ethiopia kucheza na Wolaitta Dicha FC katika mchezo wa mkondo wa pili ambapo mechi ya kwanza iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.







Kama kweki Mkwasa amehusika juu ya mambo sita yaliyoandikwa kwnye moja ya chambo cha hbr laxima awajibike kwa nguvu zote,
ReplyDeleteYanga kama wapo makini ktk utawala na uongozi wa club yao wayachunguze yale mambo sita yaliandikwa na lile gazeti la michezo yanamuhusu kocha lwandamina mambo sita yaliyo mfanya aondoke yanga na zaidi yalikuwa yanahusisha uongozi na mtendaji mkuu kama ikithibitika kuna ukweli basi wote walio husika wajitathimin na kuchukua uamuzi kwa maslahi ya club.
ReplyDeleteAondoke mipango imekuwa haina malengo na amezidi kumkumbatia ngoma ambaye hana msaada na timu
ReplyDeleteHuyo aondoke tu. Akilimali yupo wa kuivusha yanga kwa hali na mali
ReplyDeleteChonde chonde Jamani. Kuna watu huwa wanaropokwa vitu vya hovyo tu. Mkwasa kamwe hawezi kuwa mtu wa kuisaliti Yanga. Tuhuma nyingi zidi ya Mkwasa ni za kipuuzi zinazojengwa na tetesi na sio uhalisia. Mkwasa ni katibu Mkuu wa Yanga kiasi fulani yupo pale kama mlezi kwa sasa. Mkwasa anasiri nyingi za Yanga zinazohusiana na hali Mbaya ya kiuchumu inayoikabili Timu kwa sasa. Kama Mkwasa akiiacha Timu au kushinikizwa kaondoka katika kipindi hiki Yanga wakija kupigwa sita na SIMBA wasije kumtafuta mchawi. Mkwasa hapaswi kaondoka Yanga kwa sasa nakama anahasira basi anatakiwa kustahamili mpaka mwisho wa msimu. Hivi vilabu vyetu ndivyo vilivyo mara nyingi utu wa mtu huthaminiwa wakati wa faraja tu.
ReplyDeleteWacha aende anakula hela za rwandamina
ReplyDelete