Uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar, umeweka wazi kuwa hadi sasa hawajajua mechi yao ya kimataifa ya kombe la shirikisho wataicheza uwanja gani hapa nyumbani.
Mtibwa Sugar wamepangwa kucheza na Northen Dynamo ya Shelisheli katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika ambayo wanaweza kucheza kati ya Novemba 27 na 28, ipo chini ya kocha Zuberi Katwila.
Ofisa habari wa timu hiyo, Thobias Kifaru amesema kuwa mpaka sasa hawajajua ni wapi watacheza mechi yao kati ya Uwanja wa Taifa, Dar au uwanja mwingine kutokana na kutotuma sehemu ambayo watachezea.
"Ratiba tumeiona na sisi tunajiandaa vizuri kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi hiyo itakayokuwa na ushindani ila hatujajua ni uwanja gani tutautumia kwa ajili ya mechi hiyo, kama tutatumia uwanja wetu wa Manungu au Taifa, bado tunashauriana ni wapi ambapo tutacheza mechi hiyo," alisema.
Mtibwa imefuzu hatua hii baada ya kutwaa ubingwa wa kombe la FA ambao ulikuwa unashikiliwa na Simba katika fainali waliocheza dhidi ya Singida United, uliochezwa mkoani Arusha.
Kutoka Championi








0 COMMENTS:
Post a Comment