MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa sababu kubwa ya kupoteza mchezo wake mbele ya Polisi Tanzania ni kukosa umakini kwa wachezaji wake kwenye mchezo huo.
Jana Yanga ilipoteza mchezo wake mbele ya Polisi Tanzania ulochezwa Uwanja wa Ushirika Moshi kwa kufungwa mabao 2-0 ambao ulikuwa wa kirafiki.
Mabao ya Polisi Tanzania yalifungwa na Marcel Kaheza pamoja na Ditram Nchimbi na kuifanya Polisi kuibuka wababe kwenye mchezo huo.
Zahera amesema,:"Ulikuwa ni mchezo mzuri na mgumu, kila timu ilikuwa inapambana kutafuta matokeo chanya mwisho wa siku wachezaji wangu wameshindwa kuwa makini kutumia nafasi walizozipata na kuruhusu kufungwa, wakati mwingine tutaongeza umakini kupata matokeo," amesema.
Jana Yanga ilipoteza mchezo wake mbele ya Polisi Tanzania ulochezwa Uwanja wa Ushirika Moshi kwa kufungwa mabao 2-0 ambao ulikuwa wa kirafiki.
Mabao ya Polisi Tanzania yalifungwa na Marcel Kaheza pamoja na Ditram Nchimbi na kuifanya Polisi kuibuka wababe kwenye mchezo huo.
Zahera amesema,:"Ulikuwa ni mchezo mzuri na mgumu, kila timu ilikuwa inapambana kutafuta matokeo chanya mwisho wa siku wachezaji wangu wameshindwa kuwa makini kutumia nafasi walizozipata na kuruhusu kufungwa, wakati mwingine tutaongeza umakini kupata matokeo," amesema.







Ndio watawezekana akina Rollers nyumbani kwao ikiwa mambo Ni kama hayo
ReplyDeleteNadhani viporo vya Simba kwenye mechi za kirafiki ndio chanzo kikubwa kwa Yanga kufungwa na polisi Tz.
ReplyDeleteAlisahau kusema hayo maana anahisi kila anapofeli kuna mkono wa simba
DeleteHiyo ndo timu aliyoitaka. Akawatema kamsoko na Tambwe. Ameleta kalengo na lukaku wa kongo, hawafai hao.
ReplyDeleteNa bado tukutane kwenye ligi kuu bala
ReplyDeleteSishangai yanayotokea Yanga kwenye mechi za kirafiki na za mashindano ya CAF nilishashauri huko nyuma kuwa Yanga inahitaji kuliimarisha benchi la Ufundi kuongeza ujuzi na mbinu kwani viwango vya wachezaji vinaporomoka kwa kiwango cha juu mno....uwezo wa benchi la ufundi la Yanga ni mdogo mno...na kama hatua za haraka hazitachukuliwa kuliimarisha benchi la ufundi kuna hatari sana huko mbele aibu itatokea...Mimi si tu kwamba ninatathmini mchezo wa soka kwa umahiri ninazichambua timu kutokana na mechi zinazocheza.....nilisema kuwa Yanga inahitaji kuiiga Simba kutafuta Kocha Msaidizi kutoka Ulaya au Hata Amerika Kusini au Asia au Hata Africa mwenye viwango vya FIFA....ili wachezaji waongezewe mbinu katika mashindano.....Bado Yanga wana wachezaji wazuri lakini soka wanalocheza watapata tabu wakicheza na timu zenye mbinu za kubadilisha mchezo haraka.....kwahiyo hili la kubadilisha au kuliimarisha benchi la ufundi haliepukiki
ReplyDeleteKuweni wakweli mwanayanga mwenye nia njema na Yanga lazima aseme ukweli na akosoe pale ambapo panatakiwa kiukweli kuna mapungufu katika Yanga yote ukianzia mapungufu ya kiutawala, kiutendaji, kimipango na maandalizi ya michuano ya kimataifa na ya kitaifa....kuwa na mapungufu ni kitu kimoja ambacho kila timu inakuwa nacho lakini tofauti ni namna unavyochukua hatua kurekebisha makosa ya kiutawala, kiutendaji, kimfumo, kimipango na timu kwa ujumla. Yanga inahitaji mabadiliko makubwa kiuwekezaji na kimaandalizi kwa maana ya mashindano inayoshiriki benchi la ufundi lote na wachezaji lazima wabadilike pamoja na wanachama wajitolee kimali na kimawazo kufikia malengo hayo...nilisema awali na ninasema mara nyingine benchi la ufundi bado lina uwezo mdogo mno na mbinu za maandalizi ni za chini mno....nilisema kuwa lazima uwekezaji ufanyike tena haraka ili Kurudisha furaha iliyopotea Jangwani....Miundo mbinu bora na benchi la ufundi bora na usimamizi wa timu wa kisasa unahitaji uwekezaji hili halikwepeki. Nilisema kutafuta mechi za kirafiki na timu dhaifu haitaisaidia Yanga kujua mapungufu yake na itachukua muda kupata muunganiko na ndiyo yanayotokea Moshi na Zanzibar. Nilisema lazima kuwepo na mabadiliko kwenye kuinua viwango vya wachezaji kwa kupata mwalimu msaidizi wa kiwango cha juu.....kwani waliopo wamekwama kufikia ilo lengo....muda utaongea tu kudhihirisha hili. Nilisema hii dhana ya uchangiaji kwa kutegemea wananchi kuingia viwanjani kwenye mechi....kwani uwezo wa kufanya hivyo wiki mpaka wiki haupo kwani uchumi wa nchi unayumba hivyo utakwamisha jitihada kusaidia kuinua pato la klabu...ni lazima wawekezaji waingie na kumwaga fedha kwenye kukarabati miundo mbinu ya viwanja majengo na kusaidia timu za vijana na wanawake....kulipa mishahara na posho kwa wachezaji waliosajiliwa.
ReplyDelete