July 2, 2020

INAELEZWA kuwa hali ya beki wa Simba kipenzi cha mashabiki, Shomari Kapombe  sio ya kutisha sana kwani alipata majeraha kidogo kwenye mguu wake pamoja na hasira alizokuwa nazo zilimfanya ashindwe kuwa kwenye ubora wake.

Kapombe alichezewa faulo na mchezaji wa Azam FC , Frank Domayo jana, Julai Mosi Uwanja wa Taifa wakati Simba ikifunga mabao 2-0 kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali.

Habari kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa baada ya kupewa huduma ya kwanza, Kapombe aliweza kusimama na kutembea mwenyewe jambo linalomaanisha kwamba hana majeraha makubwa.

"Ilikuwa ni hali ya mshtuko aliyoipata pamoja na hofu ya kutumia ukichanganya na hasira vilimfanya awe katika hali ile ila leo atafanyiwa vipimo kwani jana aliweza kusimama  baada ya kupewa huduma ya kwanza  a kupunguza hasira," ilieleza taarifa hiyo.

Sven Vandenbroec, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa mpaka atakapochukuliwa vipimo ndipo watazungumzia hali yake.

1 COMMENTS:

  1. Yule domayo atakuwa katumwa na yanga hii ni mara ya pili alishamwumiza Boko

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic