February 20, 2021

 


KUFUATIA mabadiliko ya ratiba ya mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika kati ya Namungo na Clube Desportivo 1º de Agosto ya Angola utakaopigwa kesho, ratiba ya mchezo wa ligi kati Azam na Tanzania Prisons imebadilishwa.

Azam kesho ilitarajiwa kuwa mwenyeji wa Tanzania Prison katika mchezo wa Ligi Kuu uliopaswa kupigwa katika dimba la Azam Complex Chamazi, kabla ya ratiba hiyo kupanguliwa kutokana na mchezo huo wa Namungo.

Akizungumzia mabadiliko hayo, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Azam, Zakaria Thabith, ‘Zaka Zakazi’ amesema: “Mchezo wetu wa kesho Jumapili dhidi ya Tanzania Prisons umeahirishwa mpaka siku ya Jumatatu, hii ni kutokana na mabadiliko ya mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika kati ya Namungo na de Agosto.

Azam inaendelea kusalia katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi na pointi zao 36 walizokusanya katika michezo yao 20 waliyocheza mpaka sasa.


1 COMMENTS:

  1. Hivi wachezaji wa namungo wale walioshikiliwa angola walishaachiwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic