LAZIMA ukubali kwamba kama ukiamua kufanya kazi na wakubwa wakubwa, basi lazima ukubali kuwa na mawazo ya kikubwa na uishi maisha ya aina yao.
Klabu ya Simba imeamua kuwa klabu
kubwa si Tanzania pekee, badala yake sasa wanaangalia zaidi barani Afrika
ambako tayari kuna vigogo wake.
Safari ya Simba kutaka kuwa bora na
wakubwa barani Afrika si nyepesi na haiwezi kuwa nyepesi. Wao wanalijua hili
ndiyo maana wamekuwa na mikakati kadha wa kadha kuhakikisha wanakuwa katika
kiwango hicho wanachokitaka.
Wanajua yanahitajika mambo mengi sana
ya kufanyika ili wafikie katika kiwango hicho. Vizuri wamejipanga na unaona
hatua wanazoanza kuchukua kwenda wanapotaka zinakuwa na mashiko au mwonekano
mzuri.
Simba wanajua juu watazikuta klabu
nyingi kubwa kama Al Ahly, Esperance, Mamelodi, TP Mazembe na nyingine.
Wameonyesha kutolihofia hilo na nia yao ni kujifunza na kuendelea kukua zaidi.
Tunawaona Simba wamekuwa na mwendo
mzuri sana, unaona mfano msimu huu baada ya mechi nne za hatua ya makundi
wameshinda mechi tatu na sare moja. Unaona wameshinda ugenini mara tatu na
kutoa sare moja.
Simba ni moja ya timu ambayo
haijaruhusu hata bao moja katika mechi zake nne wakati walipocheza hatua hiyo
msimu uliopita, ndani ya mechi tatu za ugenini, walifungwa mabao 13.
Simba sasa wanakua na wanajifunza
kupitia makosa. Inaonekana watafikia mbali kwa kuwa ni wale waliokubali
kujifunza kulingana na makosa ambayo waliyafanya. Kwa kifupi, wameamua kuishi
na wakubwa na wao ni wakubwa.
Ili kuendelea kuwa wakubwa lazima
Simba wajifunze mambo mengi ya wakubwa nami nilikuwa ninawakumbusha hili suala
la kiungo wao nyota Luis Miquissone raia wa Msumbiji, kwamba kwa hapa
alipofikia anaiamsha Simba kwamba lazima waanze kujiandaa mapema wa kuziba
nafasi yake.
Bila ya ubishi, baada ya msimu huu ofa
za Miquissone zitaanza kumiminika kutoka katika klabu mbalimbali kubwa ambao
ndiyo hao wakubwa kwa kuwa wana uwezo mkubwa wa kifedha. Hiyo itawafanya wao
kuamua suala la ununuzi.
Simba wanaweza kukataa lakini ofa
ikawa kubwa na yenye ushawishi au Simba wanaweza kukataa na mchezaji akalazimisha.
Maana yake ni hivi, sasa Miquissone ni tegemeo la Simba lakini kuna kipindi
ataondoka kutokana na wakubwa wanavyotaka.
Tabia za wakubwa ni kupata vitu bora
na kama Miquissone ameonyesha uwezo, basi lazima klabu moja mbili watamuwinda,
hii maana yake Simba wanapaswa kujiandaa mapema, kwamba ikitokea wamemuuza
Miquissone ameondoka, nani atashika nafasi yake?
Kwamba wanajua wao bila Miquissone
basi watakuwa wamepungukiwa kitu, basi sasa ulikuwa ni wakati wa wao pia kuanza
“kuchungulia” katika klabu mkbalimbali kwa wake watachukua nafasi yake.
Hii ndiyo kuishi kikubwa, maana yake
unakuwa tayari wakati wowote, unapomuuza fulani basi unajua kuna fulani anakuwa
tayari kuingia na kuchukua nafasi yake.
Kujiandaa mapema ni vizuri zaidi
lakini lazima ujue suala la kufanyabiashara unapokuwa mkubwa ni zaidi ya
lazima, hauwezi kukwepa. Na vizuri kwa Simba wamekuwa wepesi kuwaachia
wachezaji wao kwenda kucheza nje au kwingine, hivyo hili haliwezi kuwasumbua.
Namtolea mfano Miquissone kwa kuwa
katika mechi nne za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, hakika
amejitahidi sana, amefanya vizuri.
Tayari anaonekana na tayari wakubwa
wengine wameshakaa vikao na kuangalia uwezo wake. Hivyo wakati wowote wanaweza
kutua Simba na kuweka dau mezani.
Wakati wa kujiandaa kwa Simba ni
sasa, kwamba kama wakifanyabiashara na wao watafanya vipi kuhakikisha wanapata
mtu na kikosi chao kinaendelea kuwa imara.
Hatari iliyopo mbele ni hivi; kama
mtakuwa mnauza tu na hakuna kusajili, au mnasajili lakini si usajil bora, basi
baada ya muda mfupi, kikosi kitashuka hadhi na uwezo na baadaye kuanza
kuboronga.







KAWAIDA AKIONDOKA SIO MBAYA, NEYMAR ALIONDOKA BARCELONA KWANI TIMU IMEKUFA KABISA? KUNA WAKATI HAUWEZI KUMLAZIMISHA MCHEZAJI ACHEZE HAPO NI KUWAKOSEA HESHIMA WENGINE PIA.
ReplyDeleteAkiondoka tutamchukua nchimbi! Haaa haaa haaa
ReplyDeleteUmeandika Vizuri
ReplyDelete