July 5, 2021


 JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa maandalizi ya timu yake kuelekea mechi zilizobaki yapo vizuri na wanaamini watapata matokeo chanya.

Mchezo ujao wa Coastal Union inayopambana kujinasua kutoka hatari ya kushuka daraja ni dhidi ya Simba  unatarajiwa kuchezwa Julai 19, Uwanja wa Mkapa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mgunda amesema kuwa ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji ushindi hivyo anaamini kwamba vijana wake watafanya vizuri.

“Vijana wapo vizuri kwani kila mchezaji anajua kwamba tunahitaji ushindi na mechi zetu ambazo zimebaki ni lazima tupambane hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti.

"Kila mmoja anahitaji kuona kwamba tunarejesha hali ya kujiamini na hilo linawezekana hasa ukizingatia kwamba kila timu inahitaji kupata pointi tatu,” amesema Mgunda.

Mchezo wao uliopita walipokutana, Mgunda alishuhudia ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ukisoma Coastal Union 0-7 Simba na hat trick ya kwanza ya John Bocco ilikusanywa hapo.

2 COMMENTS:

  1. Hawa nikuwabonda tu Hadi kuwashusha daraja

    ReplyDelete
  2. Naomba mpigwe Saba, nyinyi ni tawi la simba na kocha wenu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic