August 26, 2021


INJINIA Hers Said, Mjumbe Kamati ya Usajili wa Yanga amesema kuwa kipa ambaye amesajiliwa kutoka nchini Mali, Diarra Djigui anadaka mpaka mishale.

Nyota huyo inaelezwa kuwa amepewa dili la miaka miwili alikuwa na timu iliyoweka kambi nchini Morocco kabla ya kusitishwa na sasa timu ipo ndani ya ardhi ya Tanzania.

Injinia amesema:"Umeona ile timu ambayo tumesajili. Yule Diarra ni bonge moja ya kipa na anadaka mpaka mishale ukiachana na mpira hivyo ni usajili mzuri ambao tumefanya.

"Ukiachana na Diarra una beki Djuma Shaban, una Kibwana Shomari,Dickson Job, Bakari Mwamnyeto unadhani Mukoko, (Tonombe)," amesema.

Agosti 29 Yanga inatarajia kuwa ni kilele cha Wiki ya Mwananchi ambapo watatambulisha wachezaji wake wapya pamoja na benchi la ufundi.

7 COMMENTS:

  1. Hapo ni mazoezini ila utunze maneno yako usuje ujasena tulikunukuu vibaya, j2 sio mbali tutapata picha

    ReplyDelete
  2. Mwambie ajiandae sept 25 Kuna mabomu ya nyuklia kutoka kwa mnyama

    ReplyDelete
  3. Ameshawachota yanga haeana ujanja hata akisema lolote wataamini tuu

    ReplyDelete
  4. Kipa anadaka mshale, ha ha ha, ha angekuja huku bongo?

    ReplyDelete
  5. Ahaa Wazeee wa Haji Manara mna kiwewe,simkae kimya.

    ReplyDelete
  6. Si huyu huyu alituahidi ubingwa msimu uliopita?Ukiamini anachozungumza huyu msomali utapoteza muda wako.Mpira sio fani yake amewekwa pale na GSM kulinda maslahi yao.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic