April 20, 2013





Baada ya ushindi wa kwanza ulioambana na vituko, Sunderland chini Roberto Di Canio leo timu hiyo imeonyesha haikubahatisha.

Maana imeichapa timu ngumu ya Everton kwa bao 1-0 na kufanya mashabiki wake wachanganyikiwe kwa furaha.


Wakati mashabiki walikuwa na furaha kubwa, Di Canio raia wa Italia alijikaza kisabuni na kuacha kushangilia kwa kuteleza kama alivyofanya katika mechi iliyopita.

Safari hii aliendelea kushangilia kawaida na mashabiki wake walionyesha bango linaloonyesha kwamba hawana na shida na Jose Mourinho kwa kuwa tayari wana Di Canio.

Kocha huyo alipata wakati mgumu baada ya kutua Sunderland kutokana na kushambuliwa sana na vyombo vya habari kwamba wakati akicheza West Ham alikuwa na hisia za Kifashisti.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic