April 21, 2013





Furaha ya Watanzania kumuona Mbwana Samatta akiichezea TP Mazembe jijini Johannesburg, imezimwa na mshambuliaji Mzambia, Collins Mbesuma.

Mbesuma alifunga mabao mawili wakati Orlando Pirates ilipoichapa Mazembe kwa mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Soweto jijini hapa.
 
Mbesuma
Pirates ilipata bao lake la kwanza dakika ya pili tu, mfungaji akiwa Onyekachi Okonkwo baada ya kupiga shuti kali umbali wa mita 28.

Pirates ndiyo walikuwa wakishambulia zaidi na kuipa Mazembe wakati mgumu kwa kipindi kirefu.

Samatta nusura afunge bao katika dakika ya nane lakini hakuwa makini na kupoteza nafasi hiyo nzuri.

Mazembe walibadilika baada ya kupata dakika moja kabla ya mapumziko kupitia kwa mshambuliaji Patou Kabangu. Wakaaanza kushambulia mfulilizo.

Kipindi cha pili, Mazembe walirudi na moto tena na dakika ya 50, Rainford Kalaba alipiga shuti kali lakini halikulenga lango.


Mbesuma alifunga bao katika dakika ya 57 kabla ya kuongeza la pili kwake na la tatu kwa Pirates hivyo kuipa Mazembe wakati mgumu zaidi.

Mbesuma ndiye mshambuliaji nyota zaidi katika ligi ya hapa ambaye amekuwa gumzo katika upachikaji mabao, zaidi akitumia uzoefu na kipaji chake cha juu katika ‘kucheka na nyavu’.

Matokeo hayo, yaifanya Mazembe ilazimike kushinda 2-0 ili kusonga mbele kwa faida ya bao la ugenini, wakati Pirates kupatambana kupata angalau sare tu katika mchezo wa marudiano wiki mbili mjini Lubumbashi, DRC.

Watanzania walijitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumuunga mkono Samatta ambaye amekuwa na jina kubwa mjini hapa kutokana na mafanikio yake na Mazembe na Taifa Stars.

VIKOSI:

Orlando Pirates: Senzo Meyiwa, Happy Jele, Patrick Phungwayo, Lucky Lekgwathi, Ayanda Gcaba, Maselesa, Onyekachi Okonkwo , Tlou Segolela, Rudolf Bester (Mpho Makola 75), Khetokwakhe Masuku, Collins Mbesuma
Subs: Brighton Mhlongo, Takesure Chinyama, Ndumiso Mabena, Kheki Nzunga, Daine Klate.
 
TP Mazembe: Robert Kidiaba, Eric Nkulukuta, Kean Kasusula, Hichani Himonde, Richard Kissi Boateng, Daniel Adjei Nji, Patrick Ilongo, Trespor Mputi Mabi (Solomon Assante Wafe 76), Patou Kabangu, Rainford Kalaba, Mbwana Ally Samatta.
Subs: Aime Bakula, Gladson Awako, Nathan Sinkala, Herve Ndonga, Jonas Sakuwaha


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic