Taifa Stars imepangwa katika Kundi A la michuano ya Cosafa inayotarajiwa kuanza Julai 6 hadi 20 katika miji mitatu ya Zambia.
Pamoja na kupandwa kundi A, Stars itakipiga na Mautirius Julai 6 katika mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo itakayofanyika mjini Lusaka.
Katika hafla maalum iliyofanyika jana Ijumaa usiku mjini Lusaka, makundi mawili yamepangwa ya A na B ambayo yanajumuisha timu zilizo chini kwa ubora wa Fifa.
Sita zilizo juu kwa ubora wa viwango vya Fifa zimepangwa kucheza moja kwa moja kuanzia hatua ya robo fainali.
Zambia amepangia kuwanza michuano hiyo dhidi ya Msumbiji wakati Malawi watacheza na Zimbabwe.
Afrika Kusini watamsubiri mshindi wa Kundi A ambalo yuko Stars wakati Angola watamsubiri mshindi wa Kundi B ambalo lina Kenya.
Katika upangaji huo wa ratiba, Tanzania iliwakilishwa na ofisa kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Idd Mshangama.
Mara ya mwisho michuano ya Cosafa ilichezwa mwaka 2009 wakati wenyeji Zimbabwe walipoichapa Zambia 3-1 katika finali na kutwaa kombe.
Kwa mara ya kwanza michuano hiyo ya Codafa ilifanyika mwaka 1997 na Zimbabwe inaongoza kwa kutwaa mataji mengi zaidi ambayo ni manne Zambia, Afrika Kusini na Angola zina matatu kila moja na ndizo nchi zilizochukua mataji wakati zilizobaki hazijawahi kuonja utamu wa kombe hilo.
Makundi yako kama yafuatavyo:
KUNDI A
Tanzania
Namibia
Mauritius
Shelisheli
KUNDI B
Kenya
Botswana
Lesotho
Swaziland
RATIBA YA MICHUANO:
06/07/13 Tanzania v Mauritius 9:30 alasiri (Lusaka)
Namibia v Seychelles 12:00 jioni (Lusaka)
07/07/13 Kenya v Lesotho 8:00 mchana (Kabwe)
Botswana v Swaziland 10:00 jioni (Kabwe)
08/07/13 Mauritius v Namibia 9:30 alasiri(Lusaka)
Tanzania v Seychelles 12:00 jioni(Lusaka)
09/07/13 Lesotho v Botswana 8:00 mchana (Kabwe)
Kenya v Swaziland 10:30jioni (Kabwe)
10/07/13 Tanzania v Namibia 10:00 jioni (Kabwe)
Mauritius v Seychelles 10:00 jioni (Lusaka)
11/07/13 Kenya v Botswana 10:00 jioni (Lusaka)
Lesotho v Swaziland 10:00 jioni (Kabwe)
0 COMMENTS:
Post a Comment