Mabingwa wa Angola, Recreativo Liboro wamezidi kuchanja mbuga baada ya kuwachapa Enugu Rangers kwa mabao 3-1.
Libolo ambao ni maarufu hapa nchini baada ya kuitoa Simba katika michuano hiyo hatua ya awali, imesinga baada ya ushindi huo dhidi ya Enugu nchini Angola.
Katika mechi ya kwanza, Libolo wakiwa ugenini walifanikiwa kutoka sare ya bila kufungana, hivyo wamesogea mbele kwa ushindi huo wa mabao 3-1.
Kabla ya kuwatoa Enugu, Libolo waliwaondoa katika mashindano hayo El Merreikh ya Sudan ikiwa ni wiki kadhaa baada ya kuing’oa Simba kwa kipigo cha bao 1-0 jijini Dar na 4-0 katika mechi ya marudiano.
Timu nyingine zilizosonga mbele ni Esperance, Sewe Sports, Cotorn sports na AC Leopards.
MECHI NYINGINE ZA LIGI YA MABINGWA JUMAMOSI:
Espérance – JSM Béjaïa 1-0...mechi ya kwanza (0-0)
Séwé Sports – FUS Rabat 0-0... mechi ya kwanza (1-1)
Stade Malien – Coton Sport 0-0... mechi ya kwanza (0-3)
Entente Sétif – AC Léopards 3-1... mechi ya kwanza (4-5p) (1-3)
0 COMMENTS:
Post a Comment