November 3, 2013

ANGETILE

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah amekataa kulizungumzia suala la kuachishwa kwake kazi.


Hata hivyo akasema atafanya mkutano na waandishi wa habari ndani ya siku mbili.

“Kwa sasa siwezi kuzungumza lolote, lakini nitakutana na waandishi ndani ya siku mbili, hivyo kuweni na subira,” alisema.
Osiah ameachishwa kazi huku mkataba wake na TFF ukiwa umebaki miezi miwili.

Hata hivyo, Rais mpya wa TFF, Jamal Malinzi amesema Osiah ataendelea kulipwa mshahara wake kwa miezi yote miwili.
Nafasi yake sasa ataikaimu, Boniface Wambura ambaye ni msemaji wa shirikisho hilo.


Tayari Wambura ameishakabidhiwa kazi hiyo iliyoachwa na Osiah ambaye ni mwandishi mwenzake wa habari.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic