Kamati ya Sheria na Hadhi za
Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajia kukutana
mwishoni mwa wiki kupitia taarifa ya utekelezaji wa agizo la wanachama
kurekebisha katiba zao.
TFF tulitoa agizo kwa wanachama wetu
kufanyia marekebisho katiba ikiwemo kuingiza Kamati ya Maadili. Mwisho wa
utekelezaji wa agizo hilo ulikuwa Machi 20 mwaka huu.
Hivyo, Kamati ya Sheria na Hadhi za
Wachezaji itapokea taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo kutoka kwa
Sekretarieti, na baadaye kutoa mwongozo wa hatua inayofuata.
0 COMMENTS:
Post a Comment