Timu za Azam na Yanga ambazo
zinachuana kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa
Tanzania Bara zinashuka tena viwanjani kesho (Machi 26 mwaka huu) kuwania
pointi tatu.
Azam yenye pointi 47 itakuwa mgeni wa
Mgambo Shooting katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Mgambo Shooting ipo katika nafasi ya kumi na moja kwenye msimamo wa VPL ikiwa
na pointi 19.
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Yanga na Tanzania Prisons kuanzia saa 10.30
jioni. Yanga ipo nyuma ya Azam kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 47.
Hata hivyo, timu hiyo ina mchezo mmoja mkononi.
Tanzania Prisons ambayo ipo chini ya
Kocha David Mwamaja hivi sasa ina pointi 22 ikiwa katika nafasi ya kumi. Timu
tatu za mwisho katika ligi hiyo itakayomalizika Aprili 19 mwaka huu zitashuka
kurudi Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Ligi itaendelea tena Jumamosi (Machi
29 mwaka huu) kwa mechi kati ya Ashanti United na Oljoro JKT itakayofanyika
Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.
Jumapili (Machi 30 mwaka huu)
kutakuwa na mechi kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons (Uwanja wa Sokoine),
Kagera Sugar na Ruvu Shooting (Uwanja wa Kaitaba), Mtibwa Sugar na Coastal
Union (Uwanja wa Manungu), JKT Ruvu na Rhino Rangers (Uwanja wa Azam Complex),
Azam na Simba (Uwanja wa Taifa) na Mgambo Shooting na Yanga (Uwanja wa Mkwakwani).
0 COMMENTS:
Post a Comment