Kampuni kubwa zaidi ya nne zinapigania
nafasi ya kuidhamini timu ya Mbeya City ya jijini Mbeya kutokana na uwezo wa
timu hiyo kwa sasa.
Mbeya City imeleta Changamoto kwenye
ligi ambapo kwa sasa inashika nafasi ya tatu nyuma ya Azam na Yanga.
Katibu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, amesema
ni kweli kuna kampuni zimejitokeza kutaka kuidhamini timu hiyo kutokana na
kutambua mchango wake katika soka.
Kimbe alisema kampuni hizo zimejitokeza
kwa wingi na lengo lao kubwa ni kutaka kudhamini timu kwa kuipa vifaa vya
michezo na vitu vyote muhimu.
“Ni kweli kuna kampuni zimejitokeza kwa
kiasi kikubwa kutaka kuidhamini timu yetu na zimekuja kwa nyakati tofauti ila
siwezi kusema ni kampuni zipi kwa sababu ni mapema sana kulizungumzia suala
hilo, mambo yakiwa tayari tutaweka wazi kila kitu.
“Lakini kwa upande mwingine huenda hao
wadhamini kama tutakubaliana nao watakuwa wametusaidia sana kutokana na kuwa
na uhaba wa vifaa kama jezi ambapo
tunapewa pea mbili msimu mzima na mikiki ni mingi. Viatu pia ni pea moja ambapo havikidhi
mahitaji,” alisema Kimbe.
0 COMMENTS:
Post a Comment