March 19, 2014


Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga wamepata sare ya pili mfululizo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, leo.

Yanga iliongoza kwa dakika 83 hadi Kelvin Friday mwenye umri chini ya miaka 20 aliposawazisha baada ya kupewa pasi safi na Salum Abubakari ‘Sure Boy’ huku mabeki wa Yanga wakiwa wamempa nafasi mfungaji amchambue kipa Juma Kaseja.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, Azam FC iliifunga Yanga mabao 3-2, kinda mwingine Joseph Kimwaga akifunga bao la ushindi baada ya kipa Ally Mustapha 'Barthez' kuteleza.

Yanga waliutawala mchezo na kupata bao katika dakika ya 14 lililofungwa na Didier Kavumbagu baada ya kutokea piga nikupige kwenye eneo la lango la Yanga.


Wakati Azam FC wanasawazisha, walikuwa pungufu uwanjani kutokana na beki Erasto Nyoni kulambwa kadi nyekundu na mwamuzi Hashim.

Huku ikiwa na pointi 44, Azam FC iko kileleni na Yanga ina pointi 39 lakini ina mchezo mmoja mkononi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic