Sasa uhakika yule mshambuliaji Kpah Sherman raia wa Liberia anatarajia kutua nchini kesho akitokea Cyprus.
Sherman ameishafanya mazungumzo na Yanga, wamekubaliana kila kitu lakini ishu ni viongozi wa Yanga kutaka kumuona angalau akisukuma gozi la ng'ombe hata kidogo.
Taarifa zimeeleza kwamba anatarajia kutua nchini na mara moja atajiunga na kambi ya Yanga iliyoko katika Hoteli ya Landmark jijini Dar.
Imeelezwa Yanga itamfanyia vipimo vya afya na akifuzu, atasajiliwa kwa mwaka mmoja.
"Anajuka Jumatano (kesho), ataungana na wenzake halafu kutakuwa na zoezi la vipimo, ataangaliwa kidogo halafu mkataba utafuatia," kilielieza chanzo kutoka ndani ya Yanga jijini Dar.
Yanga imechukua uamuzi huo baada ya kuachana na mshambuliaji Mkongo wa AS Vita ambaye ameeleza ana mpango wa kwenda Ulaya.
Lakini pia imeelezwa mshambuliaji huyo ana mpango wa kujiunga na TP Mazembe.
Sherman amekuwa aking’ara nchini Vietnam na sasa Cyprus Kaskazini.
Amekuwa akifanya vema katika timu ya Cetinkaya TSK.
Akiwa na timu hiyo, aliwahi kufunga mabao matatu katika mechi tatu.
Hadi katikati ya msimu alikuwa na mabao nane na anatarajia kuwasili leo nchini.
Iwapo atatua leo, atafanyiwa vipimo vya afra ili kupata uhakika, akifuzu anaanza kazi mara moja.
Hata hivyo imeelezwa ana mkataba wa miezi minne na klabu yake na Yanga inalazimika kuuvunja kwa kulipa.
0 COMMENTS:
Post a Comment