OWINO. |
Beki David Owino maarufu kama Calabar, anatarajia kutua nchini kesho kumaliza na uongozi wa Simba.
Owino anatua nchini mchana na moja kwa moja anakwenda Zanzibar kuungana na kikosi cha Simba ili Kocha Patrick Phiri apate kumuona.
Habari za ndani kutoka Simba zimeeleza kilichomchelewesha beki huyo ambaye anatarajia kuingia mkataba na Simba ni nafasi kwenye ndege.
"Kweli amekosa nafasi kwenye ndege, angekuja leo (Jumanne). Si mbaya, atakuja kesho na kuungana na kikosi kule Zanzibar na kocha ndiye atatuambia asajiliwe au la," kilieleza chanzo.
Simba imeamua kumchukua Owino ili kujiimarisha zaidi katika safu ya ulinzi.
Inaonekana Owino kama atasajiliwa, basi ndiye ataongoza jahazi la Simba katika ulinzi katika mechi yao ya kirafiki dhidi ya Yanga, Jumamosi ijayo.
0 COMMENTS:
Post a Comment