Kiungo mkabaji tegemeo wa Simba SC, Jonas
Mkude, ameshangazwa na kitendo cha kutoitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa,
Taifa Stars kilichoitwa hivi karibuni kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya
Malawi.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwenye
Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Machi 29, wakati timu ikitazamiwa kuingia
kambini Machi 22, mwaka huu.
Mkude
ambaye amekuwa aking’ara kwenye mechi kadhaa za Simba, amesema hajui kwa nini
hajaitwa kwenye kikosi cha timu hiyo ingawa bado anashangazwa na hali hiyo
akiamini kuwa huu ndiyo muda muafaka kwake kulitumikia taifa kutokana na
mchango anautoa kwa klabu yake.
“Sijajua kwa nini sijaitwa, japokuwa
naamini huu ndiyo muda wangu muafaka sasa wa kutumika Stars lakini siwezi kujua
mwalimu anawaza nini kwa kuwa yeye ndiyo mtu wa mwisho kwenye kila kitu, ila
pia nashangaa kuna wachezaji wameitwa na kwenye klabu zao hawatumiki ipasavyo,
labda kocha anaweza kuwa na mipango ya ziada, cha msingi niitakie timu kila la
kheri tushinde huo mchezo ambao ni muhimu pia kwetu,” alisema Mkude.







0 COMMENTS:
Post a Comment