March 18, 2015

CHINI (WA TANO KUSHOTO) AKIWA NA KIKOSI CHA STAND UNITED.
Mnigeria wa Stand, Abasarim Chidiebele amesema atapambana kumfikia mshambuliaji Didier Kavumbagu wa Azam FC kwa mabao na ikiwezekana ampite.


Chidi anataka kumvuka Kavumbagu raia wa Burundi ambaye ana mabao 10 sasa katika Ligi Kuu Bara.

Chidiebele aliyewahi kufanya majaribio Simba na kuachwa, sasa ana mabao saba, hivyo anashika nafasi ya tatu kwa ufungaji nyuma ya Rashid Mandawa wa Kagera Sugar mwenye mabao nane na kinara Kavumbagu mwenye mabao kumi.

Kavumbagu alifikisha bao lake la kumi juzi Jumatatu alipofunga bao pekee dhidi ya Ndanda FC kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Saa chache baada ya kufunga bao hilo, Chidiebele akasema: “Najua Kavumbagu kafikisha mabao kumi lakini nitahakikisha napambana na kufunga katika kila mechi ili nimfikie na kumpita.”

Alisema anajua Kavumbagu anasaidiwa sana na wachezaji wenzake kufunga jambo ambalo hata katika timu yake lipo, hivyo amepanga kufunga katika kila mechi iliyo mbele yao ili aongoze kwa ufungaji.


Mechi nyingine za Stand ni dhidi ya Mtibwa Sugar, Polisi Moro, JKT Ruvu, Azam, Coastal Union na Ruvu Shooting.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic