May 7, 2015

Mashabiki wa Yanga na wale wa Azam FC, jana walianzisha uhusiano wa muda walipokutana pamoja na kushangilia kwa pamoja.

Mfano mzuri ni mashabiki maarufu wa timu hizo, Ally Yanga na Steve Kulialia waliposhangilia kwa pamoja wakati Yanga ikifungwa kwa mabao 2-1 na Azam FC kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa kwa kuwa imejihakikishia nafasi ya pili.

Mashabiki wengine wa Yanga na wale wa Azam FC walikuwa wakizunguka kila sehemu pamoja wakishangilia mechi hiyo iliyoonekana kama ya kirafiki vile.

Hata baada ya mechi hiyo, viongozi na wachezaji wa Azam FC waliungana pamoja na kushangilia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic