Homa ya
michuano ya Kagame inazidi kupamba moto kufuatia vilabu mbalimbali zinazoshirki
michuano hiyo kuanza kuwasili jijini Dar es salaam zikiwa na vikosi vyao kamili
kwa lengo la kusaka Ubingwa wa michuano hiyo.
APR ya Rwanda
tayari imeshawasili jijjini Dar es salaam, pamoja na timu za Al Shandy ya
Sudan, KMKM ya Visiwani Znzibar, huku timu za Al Malakia ya Sudan Kusini na
mabingwa mara tano wa michuano hiyo Gor Mahia wakitarajiwa kuwasili leo saa saa
10 jioni kwa ndege ya Kenya (KQ).
Kueleka
mchezo wa ufunguzi kati ya Yanga dhidi ya Gor Mahia, wenyeji timu ya Yanga
(watoto wa Jangwani) wameendelea kujifua katika uwanja wa Polisi Ufundi chini
ya kocha wake mholanzi Hans Van der Pluijm na msaidizi wake Mkwasa kuhakikisha
wanafanya vizuri katika mechi hiyo.
Gor Mahia
ambayo inafundishwa na kocha Frank Nutal raia Skotilandi, inawasili ikiwa na
kikosi chake cha kwanza kamili kilichocheza michezo 17 ya Ligi Kuu nchini Kenya
bila kufungwa, ikishinda michezo minne na sare michezo mitatu.
Wasifu wa
Azam:
Klabu ya Azam
ilishiriki kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya kombe la Kagame mwaka 2012
lakini walishangaza wengi kwa kumaliza kama washindi wa pili baada ya kufungwa
na Yanga mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali.
Mwaka jana
ilishiriki kwa mara ya pili na kuishia hatua ya robo fainali baada ya kutolewa
na Al Merriekh kwa mikwaju ya penati.
Kundi
ililopo:
Azam iko
kwenye kundi C ikijumuishwa na KCCA ya Uganda, Adama City ya Ethiopia na,
Azam inapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri mwaka huu ikiundwa na wachezaji
wengi waliokaa pamoja kwa muda mrefu.
Wachezaji wa
kuangaliwa.
Kwa upande wa
ushambuliaji inawategemea wachezaji kama Kipre Tchetche, Didier Kavumbagu.
Nahodha
mzoefu wa Azam, John Bocco bado anaweza kuwa na mchango mkubwa. Mlinzi mahiri,
Pascal Wawa anatarajiwa kuhakikisha ngome ya Azam haipitiki kwa urahisi.
Brian Majwega, Salum Abubakar na Michel Bolou ni wachezaji wengine ambao ni
nyota na muhimu kwenye timu hii.
Benchi la
Ufundi:
Benchi la
ufundi la Azam lipo chini ya usimamizi wa kocha Muingereza, Stewart Hall. Ni
mara ya tatu kwa kocha Stewart Hall kuifundisha Azam.
Bila
shaka, kocha Hall atakuwa na malengo ya kupiga hatua moja Zaidi baada ya
kukaribia kubeba taji la Kombe la Kagame miaka mitatu iliyopita.
Rekodi Kombe
la Kagame:
Azam
inashiriki Kombe la Kagame kwa mara ya tatu. Mafanikio yake makubwa ni kufika
fainali mnamo mwaka 2012 ilipolazwa mabao 2-0 na Yanga.
Wasifu wa
KCCA:
Klabu hii
inayomilikiwa na halmashauri ya jiji la Kampala ni moja ya timu kubwa Uganda
ikichuana na timu maarufu Zaidi nchini humo, SC Villa na Express.
Wakati vigogo
Sc Villa na Express wakionekana kusuasua, KCCA imeendelea kutoa makucha kwenye
ligi ya Uganda licha ya kupoteza ubingwa wao msimu uliopita.
KCCA
iliyowahi kufundishwa na Kocha msaidizi wa Azam, George Nsimbe inasifika kwa
kucheza soka la kasi, ikishambulia Zaidi kutokea pembeni.
Baada ya
kupoteza ubingwa walioshikilia mara mbili mfululizo, KCCA imejipanga upya kwa
kusajili wachezaji wapya 11 na kutema idadi kama hio ya wachezaji walionekana
kuwa mzigo.
Kundi
Ililopo:
KCCA iko
Kundi pamoja na Azam, Adama City ya Ethiopia, Malakia ya Sudani Kusini. Itakuwa
miujiza KCCA kushindwa kufuzu kwa hatua ya robo fainali kutoka kundi hili.
Wachezaji wa
kuangaliwa:
Tom Masiko ni
kati ya viungo wanaotarajiwa kung’ara kwenye Kombe la Kagame. Walinzi Saka
Mpima na Habib Kavuma ni kati ya walinzi wanaosifika kwa kushambulia licha
licha ya kuwa kazi ya kulinda lango lao.
Mtanzania,
Shaban Kondo aliyesajiliwa kwa ajili ya msimu huu mpya, anatarajiwa kuwa moja
ya mchezaji atakayetazamwa kuona nini miguu yake inaweza kufanya akiwa dimbani.
Benchi la
ufundi:
KCCA
wanaonekana kuwa na benchi la ufundi pana Zaidi kuliko timu nyingi kwenye
mashindano yam waka huu. Benchi lao la ufundi linajumuisha makocha saba chini
ya usimamizi mkuu wa Mike Mutebi akisaidiwa na kocha Sam Ssimbwa
Rekodi Kombe
la Kagame:
Ni mabingwa
mara moja wa michuano hii wakiwa wamebeba kombe hilo mwaka 1978. Mwaka
walifika katika hatua ya fainali lakini hawakubahati kupata ushindi mbele ya Al
Merriekh ya Sudani.
NB: Kesho
siku ya ijuma saa 5 kamili asubuhi, kutakua na mkutano na waandishi wa habari
katika ukumbi wa TFF uliopo Karume. Rais wa CECAFA, Rais wa TFF na makatibu
wakuu wa TFF na CECAFA watakuwepo.
Waandishi wa
habari mnaombwa kuhudhuria bila kukosa.
IMETOLEWA NA
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)








0 COMMENTS:
Post a Comment