Mshambuliaji wa Simba, Hamisi Kiiza ametamba kuwa
kikosi anachokichezea kitafanya vema kuliko wengi wanavyofikiria.
Kiiza amesema Simba imekuwa ikifanya maandalizi mazuri
wakiwa wamejichimbia Lushoto.
“Wanaweza kuona kama hatujiandai, lakini tunafanya
kila linalowezekana kuwa fiti kwa kufuata maelekezo ya walimu.
“Baadaye tutakuwa vizuri tu, acha kwanza tumalizie
maandalizi,” alisema Kiiza.
Kiiza amerejea nchini baada ya kuwa ameachwa na Yanga
na kutimka nchini.
Lakini Simba imemnasa na kumsajili kwa miaka miwili
huku Simba wakiwa wana imani kubwa kuwa atakuwa tishio katika umaliziaji.








0 COMMENTS:
Post a Comment