Dirisha la Usajili kwa wachezaji wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Ligi
Daraja la kwanza (FDL), na Ligi Daraja la Pili (SDL) linatarajiwa kufungwa
kesho Alhamis saa sita usiku.
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), linavikumbusha vilabu vyote
vinavyoshirki msimu mpya wa 2015/2015 kuhakikisha vinakamilisha usajili wa
wachezaji wao kabla ya dirisha la usajili kufungwa kesho.
Kipindi cha dirisha la usajili kwa timu za Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na
Ligi Daraja la Pili kilifunguliwa Juni 15, 2015 na kitamalizika kesho kwa awamu
ya kwanza ya usajili.
0 COMMENTS:
Post a Comment