Na Aidan
Mlimila
Waingereza
wana msemo wao mmoja wanasema "No longer at ease" ukiuleta katika
lugha ya kiswahili una maana ya "Hakuna marefu yasiyo na
ncha".Chochote kile ambacho kinakuwa na mwanzo lazima kitakuwa na mwisho
pia.
Ni mda mrefu
sasa tangu Jose Mourinho alipoanza kumnyanyasa kocha wa Arsenal,Arsene
Wenger.
Tangu mwaka 2004 Jose Mourinho alipojiunga na Chelsea akitokea Fc Porto
ya Ureno, Wenger alikuwa hajawai kumfunga Mourinho katika mechi 13 walizokutana
mpaka mwisho wa msimu uliopita Wenger alikuwa hajawai kushinda zaidi ya
kuambulia sare.
Hii ina maana
Arsene Wenger alikuwa hajawai kupata matokeo chanya dhidi ya Mourinho kwa
takribani dakika 1,170.
Mourinho amekuwa akimnyanyasa Wenger ndani na nje ya
uwanja ukiachilia mbali uwezo wa kimbinu aliokuwa nao Jose ndani ya uwanja
lakini pia ana kipaji kikubwa mno cha kuzungumza na kucheza mind games kitu
ambacho kwa kiasi kikubwa amekuwa akimshinda Arsene Wenger.
Siku ya
jumapili iliyopita tar 2 ilikuwa ni siku ambayo Wenger alikuwa anatoka kwenye
kifungo ambacho alikuwa kwa mda mrefu na ilikuwa ni baada ya kufanikiwa
kumfunga mtu ambaye amekuwa akimnyima raha na kubeba taji la ngao ya
jamii(Community Shield). Atleast kwa sasa Wenger anaweza kupumua kutoka kwenye
manyanyaso ya Mreno Mourinho.
Nikiitazama
Arsenal kwa misimu miwili hii inaonekana kuwa na mabadiliko pale wanakuwa
wanacheza mechi kubwa(Big matches) kwa misimu michache ya nyuma Arsenal
wamekuwa wakipata tabu sana kupata matokeo katika mechi kubwa hata kwa zile
mechi ambazo wao wanakuwa wamepewa nafasi kubwa ya kushinda.
Uhasama wa
Jose na Wenger ulioonekana kuongezeka sana pale Jose alipomwita Wenger
mtalaamu/bingwa wa kufeli(specialist in failure) kitu kilichopelekea wawili
hawa kushikana mashati wakati timu hizi zikipokutana pale darajani.
Wachezaji
wengi wa Arsenal kwa sasa wanaonekana kukomaa na hata ule uwoga ambao wamekuwa
nao hasa pale wanapocheza mechi kubwa kwa sasa unaonekana kuisha kitu
kinachonifanya nianze kuamini na kuona kama ule uteja ambao Wenger alikuwa nao
kwa Mourinho unaanza kutoweka kama siyo umeshatoweka.
Ingawa bado
nadhani Arsenal inabidi wafanye kazi kubwa sana ili waweze kushinda taji la
ligi kuu kitu ambacho kimekuwa kikiwasumbua kwa mda mrefu sasa tangu watwae
taji la mwisho msimu wa 2003/04.
0 COMMENTS:
Post a Comment