October 19, 2015

TEGETE (KULIA) AKIWA KATIKA MAZOEZI YA MWADUI FC
Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesisitiza kwamba mshambuliaji Jerry Tegete anaweza kurejea katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.


Julio amesema Tanzania bado ina tatizo la wafungaji na Tegete ambaye ameanza kuonyesha cheche zake kwa kufunga bao katika mechi yao iliyopita ana nafasi ya kurejea Stars kama atajituma zaidi.
 “Tegete amefunga bao zuri sana, utaona kuwa ana kipaji na suala la uwezo wake si kitu kigeni.
“Kama atajituma zaidi mazoezi na katika mechi, basi ana nafasi ya kurejea Taifa Stars,” alisema.
 Tegete amejiunga na Mwadui FC baada ya kuachwa na Yanga ambayo ilimuweka benchi kwa zaidi ya miezi minne.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic