Kiungo mshambuliaji wa Royal Eagles ya Afrika Kusini,
Uhuru Selemani sasa amegeuka lulu nchini Afrika Kusini.
Uhuru amekuwa lulu baada ya baadhi ya klabu za Ligi
Kuu Afrika Kusini ikiwemo Mamelodi Sundown kuendelea kumfuatilia.
Mmoja wa mtandao wa Afrika Kusini, umesema kwamba
Uhuru ambaye anatumia jina la Mwambungu, amekuwa kivutio cha timu kubwa.
Kichwa cha habari cha taarifa hiyo kimeeleza hivi;
“Mwambugu now is a target for big fish”, yaani Mwambungu sasa anatupiwa macho
na timu kubwa.
Tayari Uhuru aliyewahi kuzichezea Simba, Coastal
Union, Mtibwa Sugar na Mwadui FC ameshaanza kuonyesha uwezo wa kufunga akiwa na
Royal Eagles inayoshiriki darala la kwanza.
Kiungo huyo Mtanzania anaichezea Royal Eagles akitokea
Jomo Cosmos.
0 COMMENTS:
Post a Comment