Kikosi
cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro Premium Lager, kimeondoka leo saa 4 asubuhi kuelekea nchini Afrika
Kusini kuweka kambi ya siku 10 kujiandaa na mchezo dhidi ya Algeria Novemba 14
jijini Dar es Salaam.
Taifa
Stars imeondoka kwa usafiri wa Shirika la Ndege la Fastjet ikiwa na kikosi cha
wachezaji 24, pamoja na bechi la ufundi linalongozwa na Kocha Mkuu Charles
Boniface Mkwasa.
Wachezaji waliondoka
ni Ally Mustafa, Aishi Manula, Said Mohamed, Juma Abdul, Shomari Kapombe,
Ramadhan Kessy, Mohamed Hussein, Haji Mwinyi, Hassan Isihaka, Salim Mbonde,
Kelvin Yondani na Nadir Haroub.
Wengine ni Mudathir
Yahya, Frank Domayo, Himid Mao, Salum Abubakar, Farid Mussa, Saimon Msuva,
Salum Telela, Jonas Mkude, Said Ndemla, Ibrahim Hajibu, Malimi Busungu na John
Bocco.
Mshambuliaji wa
Stand United, Elias Maguli anatarajiwa kuungana na kikosi hicho kesho baada ya
kuitumikia timu yake katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom leo jumatatu
dhidi ya Mgambo Shooting katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Aidha washambuliaji
Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Mrisho Ngasa wanaocheza soka nje ya nchi,
wataungana na wenzao baada ya michezo ya mwishoni mwa wikiendi hii.
0 COMMENTS:
Post a Comment