March 7, 2016


Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, amesema kuwa dakika 15 za mwanzoni zilitosha kabisa kuwamaliza wapinzani wao, Azam FC, kwenye mechi ya jana.

Yanga ilivaana na Azam kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na mechi kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Kwa sare hiyo, timu hizo zilizopo kwenye mbio za ubingwa, zina pointi sawa (47), zikitofautiana kwa mabao.

Pluijm alisema timu yao ilishindwa kutumia nafasi za kufunga mabao katika dakika hizo za mwanzo ambazo kama wangezitumia vyema, basi mechi isingemalizika kwa sare.

Pluijm alisema bado ana tatizo kwenye safu la ushambuliaji, inayochezwa na Mzimbabwe, Donald Ngoma na Amissi Tambwe, hivyo amepanga kuiboresha safu hiyo kuhakikisha wanapata mabao mengi.

“Katika mechi ya leo (juzi) dhidi ya Azam tunatakiwa kujilaumu wenyewe kutokana na kushindwa kuzitumia nafasi nyingi tulizokuwa tunazipata katika dakika 15 za mwanzo.

“Hivyo kama kocha nimeliona hilo tangu mechi na Simba, nimepanga kulifanyia kazi kuhakikisha tunafunga mabao mengi mechi zijazo za ligi kuu,” alisema Pluijm.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic