March 6, 2016




 
Benteke akishangilia baada ya kutupia bao la ushindi.
Liverpool ikicheza na wachezaji 10 kwa dakika nyingi uwanjani, imelazimika kutoka nyuma kwa kufungwa bao 1-0 na kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace katika Ligi Kuu ya England ‘Premier League’ kwenye Uwanja wa Selhurst Park.

Liverpool ambayo kutokana na ushindi huo sasa imefikisha pointi 44 na kushika nafasi ya saba katika msimamo wa Premier, ilicheza pungufu muda mwingi kutokana na kiungo wake mkongwe James Milner kupewa kadi ya pili ya njano katika dakika ya 63.

James Milner (kushoto) akitoka uwanjani baada ya kupewa kadi nyekundu.
 
Crystal Palace ilipata bao lake katika dakika ya 49 kupita kwa Joseph Ledley wakati ambapo Liverpool ilisawazisha katika dakika ya 72 kupitia kwa Roberto Firmino.

 
Wachezaji wa Liverpool walimpongeza Firmino baada ya kusawazisha bao.
 
Firmino

Bao la pili lilipatikana baada ya Christian Benteke kuchezewa faulo katika dakika za lala salama kisha yeye mwenyewe kuutupia mpira wavuni. 



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic