July 10, 2016

MUDA MCHACHE BAADA YA AJALIBeki wa zamani wa Simba, Emily Mugeta amenusurika na kifo baada ya ajali mbali ya gari iliyotokea juzi nchini Ujerumani.

Dereva aliyekuwa akiendesha gari alilokuwa akisafiria Mgeta alifariki dunia papo hapo.

WAKATI AKISAINI SIMBA...
Akizungumza na SALEHJEMBE, Mgeta anayekipiga katika timu ya daraja la nne ya Neckarsulmer.

“ Ilikuwa ni baada ya mechi, ajali imetokea kama saa sita usiku hivi baada ya kumshinda dereva na kugonga kuta za uzio za barabara na kupinduka mara mbili.

WAKATI AKISAINI NECKARSULMER
“Tulikuwa tunatokea eneo linaitwa Neckarsulm tunarudi Heilbronn, ndiyo ajali ikatukuta,” alisema Mgeta.

“Bahati mbaya tumempoteza mwenzetu aliyekuwa akiendesha, mwingine amelazwa. Mimi mbavu zinaniuma sana, nilipata matibabu na kuruhusiwa lakini bado ninasikia maumivu makali.”

ALIPOTAMBULISHWA NECKARSULMER

Mgeta alijiunga na timu hiyo ya Ujerumani akitokea Polisi Morogoro ambayo hata hivyo hakuichezea baada ya kujiunga nayo akitokea Simba ambayo ilimsajili miaka mitatu minne iliyopita.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV